Sunday, March 18, 2012

HASHIM THABIT ATINGA KLABU NYINGINE NBA.

 
MCHEZAJI wa kulipwa wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hasheem
Thabeet amechukuliwa na klabu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki kwenye Ligi
ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA) kutoka klabu ya Houston Rockets.
 
Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mitandao mbalimbali yaintaneti, Portland Trail Blazers imefanikiwa kumnyakua Mtanzania huyo kutokaRockets kwa kubadilishana na mchezaji mwingine Marcus Camby, jana ambayo ilikuwasiku ya mwisho iliyowekwa na NBA kwa ajili ya klabu zinazocheza ligi hiyo kufanyautaratibu huo wakubadilishana wachezaji.
 
Mlinzi Jonny Flynn, pia amejiunga na klabu ya PortlandTrail Blazers kama sehemu ya utaratibu huo, Thabeet ambaye sasa amechukuliwa na Blazers kabla alichukuliwa na Houston Februari mwaka jana, akitokea Memphis na alifanikiwa kuichezea Rockets mechi tano pekee
katika msimu huu wa ligi.
 
“Tunatazamia kuwa yale yatakayofanywa na Jonny pamoja na
Thabeet yanaweza kuleta mafanikio katika timu yetu na pia tunamshukuru Marcus
kwa mchango alioutoa kwa kipindi cha misimu mitatu aliyokuwa nasi na tunamtakia
kila la heri huko alikoenda,” alisema Kaimu Meneja Mkuu wa Blazers Chad
Buchanan.
 
Katika michezo 120 ya misimu mitatu akiwa na klabu za
Memphis na Houston, Thabeet mwenye umri wa miaka 25, ana wastani wa pointi 2.2,
na jumla ya dakika 10.7 pamoja na rebaundi 2.

No comments: