Wednesday, March 14, 2012

JIJI LA RAHA NA KARAHA LINAITWA DAR ES SALAAM.

 Chemba ya maji taka ikiwa imeondolewa mfuniko wake na kuliacha shimo kubwa linalohatarisha watumiaji wa barabara ya umoja wa Mataifa karibu na makutano ya barbara hiyo na barabara ya Morogoro eneo la Fire. Gari kama hili pichani pata picha kama ni usiku linatumbukia tutasema ni bahati mbaya?
 Dimbwi hili kubwa la maji taka limekua likiwasumbua wakazi wa jiji la Dar es Salaam wa eneo la Kariakoo barabara inayoelekea Hospitali ya Regency karibu na Makutano ya barabara hiyo na ya Umoja wa Mataifa. Kuna hitajika hatua za haraka ya kuliondoa dimbwi hilo kwa kulinda afya za wakazi wa eneo hilo na hata wanafunzi wanao tumia barabara hiyo.

No comments: