Tuesday, March 13, 2012

KILWA HAIJAPATA HATA SENTI KUTOKANA NA GESI YA SONGOSONGO.


WAKATI naandika ripoti maalum kuhusu Kilwa nilisema kunahitajika mwamko mkubwa kwa watu Kilwa ili kuharakisha maendeleo.
Lakini nikasisitiza mwamko huo utatokana na watu wakilwa wenyewe waliopo hapo kwa kushirikiana na walio nnje ya mji huo.
 Jana nilishitushwa mno na Taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia kituo kimoja cha Televisheni na Radio, akilalamika kuwa tangu kampuni ya Panafrican Energy, ianze kazi ya kuzalisha gesi wilayani humo na hawajapata hata shilingi moja kutoka kwa kampuni hiyo inayoshirikiana na kampuni ya Songas kwa upande wa miundombinu ya kusafirisha gesi. Na kutokana na kukosa pesa hizo Wilaya hiyo hupoteza zaidi ya Tsh.1Billioni na kubaki mapato kiduchu tu ya Wastani wa Tsh.300Millioni tu.
Kitu cha kuchefua zaidi kwenye taarifa hiyo ni kwamba walipokwenda kuzidai pesa hizo kwenye kampuni hiyo wakajibiwa pesa hizo hulipwa Manispaa ya Ilala kwakuwa ofisi za kampuni hiyo zipo  Ilala! Jamani wenzangu mnasemaje kwenye hili. Tujadili.

JUHUDI ZA KUWASAKA WAHUSIKA WOTE ZINAENDELEA, NITAWALETEA TAARIFA KAMILI KUHUSU HILI MSIJALI.

No comments: