Tuesday, March 20, 2012

LEO NI SIKU YA FASIHI SIMULIZI DUNIANI, Unafahamu nini? Umefanya nini kuhusu fasihi kwenye siku hii ya leo? Kama hakuna ungana nami tutabaruku japo kwa uchache.

Wataalam wa fasihi simulizi ya lugha ya Kiswahili Mzee Adam Shafi (kushoto) na Mze Andanenga wakiwa kwenye stgudio za Radio one.
 Mtaalamu wa fasihi Simulizi raia wa Nigeria Chinua Achebe.
Mze Adam Shafi.

HUWEZI kutaja fasihi simulizi bila kutaja majina haya nchini Tanzania na barani Afrika kwa Ujumla.
Leo ikiwa ni Siku ya Fasihi simulizi duniani lakini watanzania tuko wapi hakuna tunachosikia masikioni mwtu tumekaa kimya kabisa kana kwamba tupokwenye kilele cha mafanikio ya tamaduni zetu kiasi ya kusahau kabisa kule tuliko toka.


Binafsi sitaki kuwa sehemu ya hao watu najitoa kivyangu kukumbuka mengi juu ya FASIHI SIMULIZI kama utakuwa tayari ungana nami katika kutabaruku japo kwa uchache.


NINI Maana ya fasihi simulizi? 

Fuatilia somo zima.


Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia mdomo (tofauti na maandishi kama kwenye fasihi andishi) kama njia kuu maalum kwa ajili ya kufikisha ujumbe.
Ni sehemu ya msingi ya utamaduni, na vipengele vyake vingi vinafanya kazi kama katika fasihi kwa jumla.
Katika jamii isiyo na uandishi ni wazi kuwa hakuna fasihi andishi. Hata hivyo kila jamii ina hazina ya mapokeo yapokelewayo mdomo kwa mdomo—kwa mfano utenzi, ngano au nyimbo za jadi—hivyo vyote ni sehemu za fasihi simulizi.
Hata jamii ijuayo kusoma na kuandika inaendelea kuwa na fasihi simulizi, hasa nyumbani, k.m. katika kuwasimulia watoto hadithi.
Hata hivyo, mara nyingi fasihi simulizi ya jamii ijuayo kusoma na kuandika ni tofauti sana na fasihi simulizi ya jamii isiyo na uandishi, kwa vile imeathiriwa na ujuzi wa kusoma na kuandika, na mitindo ya masimulizi yake haiendi sambamba na mitindo ya masimulizi yasiyoathiriwa na uandishi.

FASIHI SIMULIZI:
Hii ni sanaa itoayo maudhui yake kwa kutumia lugha ya maneno ambayo hutamkwa au kutendwa.

Makala ya Fasihi Simulizi:
  i)Lugha ndiyo itumiwayo fanani.
  ii) Matumizi ya maneno kisanaa.
  iii) Huonyesha hisia za binadamu.
  iv) Hufunulia shughuli na kazi za watu husika.
  v) Huonyesha uhusiano baina ya binadamu na mwingine.
  vi) Humtazama binadamu na mazingira yake.
  vii) Huwajenga watu kitabia.

Umuhimu wa Fasihi Simulizi:
   i) Hutuwezesha kuelewa utamaduni na historia yetu vyema.
   ii) Husaidia katika elimu ya jamii.
  iii) Husaidia katika uga wa siasa- ulumbi
  iv) Hukuza ufasaha na ustadi wa mtambaji.
  v) Hufurahisha na kuburudisha.
  vi) Huendeleza umoja na utangamano.
  vii) Hukuza mtalaa wa lugha.
  viii) Huipa jamii mwelekeo na nasaha kwa kuonya na kushauri.
  ix) Hukuza upeo wa wanafunzi.
  x) Hufunza mbinu za sanaa na uchambuzi.
  xi) Kupokezana utamaduni wa jamii.
  xii) Kukuza maadili katika jamii.
  xiii) Ni kazi kwani watu hupata malipo kutokana na fasihi.
  xiv) Huwazindua watu ili wajue haki zao.
  xv) Hurekebisha tabia.

Sifa bainifu za uwasilishaji wa Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi:


Fasihi Simulizi                                          Fasihi Andishi
1. Huwasilishwa kwa mdomo                     -Hutegemea maandishi yasomwayo
2. Hadhira huwasiliana na mwasilishaji        -Si lazima hadhira iwasiliane na msimulizi
3. Hadhira huweza kuchangia                     -Hadhira haina njia ya kuchangia usimulizi
4. Humilikiwa na jamii                                 -Ni milki ya mtunzi au mwandishi
5. Ina tanzu nyingi                                      -Haina tanzu nyingi
6. Sifa zisizo za lugha kutumika                  -Hutegemea sifa za lugha isipokuwa igizo
7. Huonyesha ubunifu mpya                       -Hubakia kama ilivyoandikwa na mtunzi
8. Huifadhiwa akilini kwa kukumbuka           -Huifadhiwa kwa maandishi vitabuni
9. Huweza kubadilishwa (ufaraguzi)             -Msomaji hana uhuru wa kubadilisha
10. Msamiati wa utungo kupotea                 -Kazi hubakia kama ilivoandikwa
11. Kuambatanisha na utendaji                    -Haiambatanishwi na utendaji ijapo’ igizo
12. Hutumia wahusika changamano              -Hutegemea sana wahusika binadamu


Muainisho wa Fasihi Simulizi:
    Tanzu nne kuu za Fasihi Simulizi ni:
    a) Hadithi/ Simulizi-hutumia lugha nathari
    b) Maigizo-uwasilishaji mbele ya hadhira
    c) Semi- ufupi wa kimuundo
    d) Ushairi- uimbaji na muundo maalum

Vipera vya Tanzu hizi:
 
a) Hadithi/ Simulizi         b) Maigizo
i) Migani/ mighani                    I) Michezo ya jukwaani
ii) Hekaya                               ii) Mazungumzo
iii) Khurafa/ hurafa                    iii) Vichekesho
iv) Ngano za mazimwi             iv) Ngomezi
v) Soga                                  v) Ulumbi
vi) Ngano za mtanziko            iv) Malumbano ya utani

c) Ushairi                     d) Semi/ Tanzu-bainifu
i) Nyimbo                                    I) Methali
ii) Ngonjera                                 ii) Nahau
iii) Sifo                                        iii) Misimu
iv) Maghani                                 iv) Misemo
v) Majigambo                              v) Lakabu
vi) Vitendawili
vii) Vitanza-ndimi

No comments: