Sunday, March 11, 2012

MAPOKEZI YA LIPUMBA YATIKISA JIJI LA DAR, DK. Slaa asmpokea Lipumba kiaina, Baadhi ya Watu waumia, Ajali mbili zatokea.

 JIJI  la Dar es Salaam leo lilikuwa kwenye hekaheka kubwa baada ya msafara mrefu wa mapokezi ya Profesa Lipumba Kusababisha baadhi ya barabara kutopitika kabisa kwa zaidi ya masaa 6. 

Baadhi ya watu walipata ajali Lori kuanguka eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mapema kabla Profesa ajawasilina inasadikiwa watu watatu wameumia na kulazwa Hospitali.

Wakati huo huo Msafara mwengine wa cHama hicho uliokuwa ukitoka Mkoa wa Pwani ulisababisha ajali ya kugonga mtu waakati wa kielekea jijini Dar. 

Dk. Slaa Naye akitokea safari zake akakumbana na wafuasi wa Chama Cha CUF akakabidhiwa bendera ya picha ya Prof. Lipumba huku akiimbiwa nyimbo kuwa Slaa ameipenda CUF na kusindikiza hadi kwenye gari lake. 

ANGALIA PICH ZAIDI.


 Mpiga Picha wa Star tv akiwa kazini wakati kituo hicho kikirusha matangazo ya LIVE ujio huo wa Mwenyekiti wa Chama hicho.
 Mitaa ilifurika watu huku wakimpungia mikono Mh.Prof. Lipumba.


 Vijana wa CUF wakiwa na Mwenyekiti wa CUF kwenye Msafara ulioanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kupitia Tazara hadi Ubungo na kunyoosha hadi Kariako na kumaliza msafara huo eneo la Karume.

 Dk.Slaa akiwashangilia wafuasi wa CUF huku yeye akinyoosha bendera ya Prof. Lipumba.


 Saa moja kamili msafara huo ulikua eneo la Manzese darajani

No comments: