Wednesday, March 28, 2012

MREMA AICHANACHANA MANISPAA YA KINONDONI.

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) amewakemea vikali viongozi wa Manispaa ya Kinondoni na kuwataka kuwa makini kwenye uandaaji wa taarfifa za matumizi ya fedha za wananchi.

Kauli hiyo ilitokana na viongozi wa Manispaa hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Fortunatus Fwema, kuwasilisha hesabu zenye kasoro nyingi kiasi ya kuwachanganya wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo taarifa za utekelezaji wa miradi karibu yote zinakasoro mbalimbali ikiwemo suala la matumizi ya pesa kuliko kiwango kilicho kadiria hali iliyowafanya wajumbe kuhoji chanzo cha pesa hizo ambacho hakijaonyeshwa kwenye taarifa hiyo.

Aidha nae makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Iddi Azani, aliwataka wataalamu wa manispaa hiyo washirikiane ili kuhakikisha kunakuwepo na utekelezaji wa miradi unakuwepo.

WAKATI huohuo kamati imegundua kuwepo kwa matatizo ya ukusanyaji wa kodi za majengo kunakofanywa na malaka ya mapato nchini TRA na kusema watafuatilia kwa karibu kama wataona ipo haja ya kurudisha kazi hiyo kwa halmashauri zenyewe.

"Tulikwenda Temeka na Ilala tumekuta tatizo hilo Serikali na Halmashauri zilihisi kwa kuwapa TRA kazi hiyo ingekuwa na ufanisi mkubwa lakini ni kinyume chake bora zingefanywa na halmashauri zenyewe, tutaangalia namna tutakavyo lishughulikia jambo hili, alisema Mrema.

No comments: