Tuesday, March 20, 2012

MUZIKI UKIKOLEA HAIJALISHI WEWE NANI! Je Unaswali?

Wanafunzi wa Shule za Msingi za Kata ya Kipawa wakiserebuka kimtindo wakati wa harambee ya uchangiaji wa pesa za kuboresha miundombinu ya Shule za kata hiyo.
 Na sisi tumo banaaaaaaaaaaaaaaaa wacha tuonyeshe maujjuzi.

TABARUKU:

HAFLA hii ilifanyika Mwishoni mwa wiki kwenye kata ya Kipawa jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Mama Salma Kikwete, ambapo wadau mbalimbali walishiriki katika kuzisaidia shule hizo kuboresha miundo mbinu.
Hata hivyho kuna mambo kadhaa nyuma ya panzia huwa yanajitokeza hatuna budi kuyaangalia kwa jicho la pili.

Enzi zileee za miaka 30 iliyopita tungeweza kushuhudia vituko vya namna hii vya watoto? sawa maisha na mazingira ya muda ule na sasa ni tofauti lakini jamii yetu iangalie vizuri haya maadili yetu namna bora ya kuyalinda pasipo kuharibu mandeleo yetu.

Tunafahamu fika burudani ni sehemu ya utamaduni ambayo kimsingi tunahitaji kuiboresha lakini kama tunavyo fahamu kila kitu kina mahalapake.

WAKATABAHU:

No comments: