Monday, March 19, 2012

MWAKYEMBE AANZA KAZI RASMI, Alonga na waandishi wa habari.


Naibu Waziri wa Ujenzi Dk Harison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana alipofika ofisini kuanza kazi rasmi, baada ya hali yake kiafya kuwa nzuri tangu alipolazwa nchini India kutokana na ugonjwa wa uliokuwa ukimsumbua.
Naibu Waziri wa Ujenzi Dk. Harison Mwakyembe akiwasili ofisini kwake leo asbuhi kuanza kazi rasmi, baada ya hali yake kiafya kuimarika tangu alipolazwa nchini India kutokana na ugonjwa ukimsumbua.

TAARIFA KAMILI.

MWAKYEMBE anasema amepona maradhi yaliyokuwa yanamsumbua yupo fiti anaendelea na majukumu yake kama kawaida.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo alisema kuwa, sasa hivi amepona na kwamba amegundulika anasumbuliwa  na ugonjwa wa ‘Popular Throlema’ uliyosababisha kuharibika kwa ngozi yake.

“Nimerudi juzi kutoka nchini India ambapo Daktari wangu ameniambia nimepona, nilikuwa nasumbuliwa na maradhi ya ‘Popular Throlema’iliyosababisha ‘skin disorder’,”lakini kwa nguvu za Mungu nimepona, namshukuru,”alisema Dk mwakyembe.

Aliongeza shinikizo la rais Jakaya Kikwete limechangia serikali kumpa kipaumbele katika matibabu yake,jambo ambalo limesababisha kufika hapo alipo.

Alisema kutokana na hali hiyo amewataka wananchi wote kwa ujumla wakiwemo wajimboni kwake Kyela kuondoa wasiwasi kutokana na matatizo yake na kwamba yupo fiti kwa ajili ya ujenzi wa majukumu ya taifa.

“Ninaomba wapiga kura wangu wa Kyela waache jazba,wawe na subra, juu ya matatizo yangu,wiki ijayo nitakwenda kuzungumza nao ili niweze kuwaeleza matatizo yaliyokuwa yananisumbua, lakini sasa hivi niko fiti,”alisisitiza.

Alibainisha, mpaka sasa Jeshi la polisi kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Shamsi Vuai Nahodha wameunda tume ya kuchunguza matatizo yanayomsumbua, hivyo basi amewataka


MWISHO>

No comments: