Saturday, March 3, 2012

NETIBOLI LINDI HOI KWA BANDARI DAR

 Mbunge wa viti maalum Merry Mwanjelwa, akiwasalimia wachezaji wa timu ya RAS ya Lindi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mpambano wao dhidi ya timu ya Bandari ya Dar es Salaam, hadi blog inatoka uwanjani RAS ilikuwa imeshafungwa magoli 25 kwa 5.

 Wachezaji wa Lindi wakimsikiliza Mbunge wa viti maalum Merry Mwanjelwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kufunga mashindano ya ligi ya Netboli daraja la pili taifa jijini Dar es Salaam.


 Wachezaji wa bandari wakiigaragaza timu ya RAS Lindi bila huruma.
 Kikosi Kinachotarajiwa kuwa cha timu ya taifa ya Netiboli (rangi ya kijani) wakipimana ubavu na wachezaji wa timu ya Netiboli ya Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi (rangi nyekundu) jijini Dar es Salaam. Hata hivyo kikosi hicho kilibugizwa mabao 6-2 na watoto wa Bayi.

No comments: