Saturday, March 3, 2012

UBALOZI WA UHOLANZI NCHINI WAMWAGA MSAADA

Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza, akipokea msaada wa Laptop kutoka kwa Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Renet Van der Waals kwa niaba ya Chama cha Wakulima wa Maua Matunda na Mbogamboga (TAHA) kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Jumla ya Vifaa vilivyokabidhiwa vinathamani ya Tsh.100Millioni, ambavyo vitatumika kufanyia uchunguzi wa mazao ya kilimo.


 Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chama cha CHADEMA akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu malalamiko ya chama hicho juu ya ukiukwaji wa sheria za uchaguzi kwenye chagozi ndogo zinazotokana na sababu mbalimbali ikiwemo ciongozi wake kufariki. Chama hicho kina lalamika kutokana na kutofuatwa kwa taratibu za uchaguzi nchi nzima.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanzishwa kwa Tuzo mpya ya Heshima ijulikanayo kama Tuzo ya Maisha kwa waandishi waliobobea na kujutuma kwa muda wao wote kwenye taaluma hiyo kwa kufanya kazi ya kufichua uozo na kulitetea taifa. Majina Matatu yamependekezwa kupambana baada ya mchakato mrefu ambao ni Eda Sanga, Benkiko na Filli Karashani.
Waandishi wakiwa kazini kufuatilia matukio.

No comments: