Thursday, March 22, 2012

RAIS SHEIN AFANYA ZIARA MKOA WA MJINI MAGHARIBI.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na  wafanyakazi wa mamlaka ya Maji,(ZAWA) alipofika Selem katika uzinduzi wa Mradi wa
Mfenesini-Bumbwini Mkoa wa mjini Magharibi,akiwa katika ziara ya kutembelea maendeleo ya Mkoa huo,iliyoanza jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa Skuli ya Kianga,Wilaya ya Magharibi jana,(kulia) Mkuu wa Wilaya Magharibi Hassan Mussa Takirima,akiwa katika ziara ya maalum ya wilaya hiyo kutembelea mambo mbali mbali ya maendeleo.
Baadhi ya wananchi  wa Shehia za Mfenesini na Bumbwini na vitongoji vyake wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi hao wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Maji safi wa Mfenesini- Bumbwini,Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi,zilizofanyika jana huko Selem Wilaya ya Magjaribi Unguja.

No comments: