Friday, April 20, 2012

ANNE MAKINDA ABADILI KAULI, Baada ya Tundu Lissu na John Mnyika Kuomba Muongozo.

Mara baada ya kikao Cha Bunge kumalizika hivi punde Mbunge wa Singida Mashariki alisimama kutaka muongozo wa Spika kuhusu Suala linaloendelea kwenye bunge hilo la kukusanya Saini za wabunge wapatao 70 ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Lisu alidai kuwa kitendo cha Spika kutoa uamuzi kwa jambo ambalo halijamfikia mezani kwake ni kama ukiukwaji wa kanuni na sheria na itaonyesha kuwa kuna majibu yanaandaliwa kujibu hoja ambayo hatakuiona bado hajaiona na kwa kufanya hivyo nikukiuka taratibu.

Makinda alidai kuwa hajasema kwamba suala hilo si halali kufanyika ala alichosema halitawezekana kwa kikao hichi cha bunge kwasababu linaishia Juma tatu, kwahiyo itakuwa ni vigumu sana kulifanya jambo hilo ndani ya bunge hili.

Aidha akitoa ufafanuzi zadi mara baada ya Mbunge wa Ubungo 
John Mnyika, kusimama na yeye akitaka muongozo juu ya jambo hilohilo kwamba kuna tatizo gani kama watu wakiendelea kusaini (saini ambazo Mnyika alisema idadi yake imefikia 66 ) na kuwasilisha hoja siku ya juma tatu kwaajili ya kujadiliwa bunge lijalo?


Anne Makinda alisema kwamba yeye hajasema kwamba jambo hilo halifai, "Naomba nieleweke na answered zitaletwa saivi nilicho kisema! nikwamba suala hilo haliwezekani kwa bunge hili kwakuwa jumatatu ndio linafikia kikomo lakini kama mtaleta kwa kikao kijacho hakuna tatizo" alisema Makinda.

BUNGE LITAENDELEA KESHO ASUBUHI JUMAMOSI .

No comments: