Sunday, April 15, 2012

ASKOFU MPYA DAYOSIS YA ZANZIBAR ASIMIKWARais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein, akiteta jambo na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Willium Mkapa, wakati wa Ibada  maalum ya
kuwekwa Wakfu Padre Michael Henry Hafidh, kuwa Askofu wa Dayosisi ya Zanzibar jana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimkabidhi kitabu cha utambulisho cha Sheria na Sera ya Uhakika wa Chakula na Lishe   Mwakilishi wa Shehia ya Pujini
na Mbuzini Pemba, Fatma bakari Hamadi,wakati wa uzinduzi wa Baraza la Kamati za uhakika wa Chakula na Lishe katika ngazi ya Taifa,Wilaya na Shehia, huko Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar jana.

Askofu Mkuu wa Dayosisi Tanzania Dr.Valentino Mokiwa,(kushoto) akimuweka Wakfu Padre Michael Henry Hafidh,kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar Kanisa Kuu la   Mkunazini, Mjini Unguja jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Maaskofu mbali mbali wakati alipowasili katika Kanisa Kuu la Mkunazini kuhudhuria katika ibada ya kuwekwa Wakfu Padre Michael Henry Hafidh,kuwa Askofu wa Dayosisi ya Zanzibar.
Baadhi ya waumini wa Dini ya kristo Kanisa la Mkunazini Zanzibar,wakiwa katika sherehe ya kuwekwa wakfu Padre Michael Henry Hafidh,kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar,sherehe hizo zilifanyika jana katika Kanisa Kuu la Mkunazini Mjini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi kitabu cha utambulisho cha Sheria na Sera ya uhakika wa Chakula na Lishe kwa Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Uhakika wa Chakula na Lishe,ikiwa kama ni ishara ya uzinduzi wa Baraza la Kamati za uhakika wa Chakula na Lishe katika ngazi ya Taifa,Wilaya ya
Shehia,huko Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar jana.

Baadhi ya wajumbe wa  Kamati mbali mbali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wajumbe hao wakati wa uzinduzi wa Baraza na kamati za Uhakika wa chakula na Lishe katika ngazi ya Taifa huko Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.


No comments: