Tuesday, April 17, 2012

DK. SHEIN ZIARANI PEMBA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Afani Othman Maalim, alipotembelea Bonde la Ukele,kukagua Tuta la kuzuia Maji Chumvi,katika Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba,akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya jamii katika Wilaya hiyo.Askari wa Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) na Mafunzo wa Pemba wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na kikosi kazi na kutoa  shukurani kutokana kufanikisha zoezi la uchumaji wa karafuu ambao umepelekea kuongezeka kwa mapato kwa Serikali ya Mapinduzi,sambamba na kuimarishwa kwa ulinzi katika zoezi hilo,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Pemba.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha Afya Chimba, Jimbo la Tumbe, alipokuwa ziarani kuangalia maendeleo ya jamii katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wananchi na Wanachama wa Chama cha  Mapinduzi CCM wa Tawi la Pobwe Magharibi,Wete Pemba
alipofika kuzindua Tawi la CCM katika kijiji hicho,alipokuwa katika ziara maalum ya kuimarisha Chama.Baadhi ya wananchi wa Chimba Kaskazini Pemba, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza nao wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha Afya katika Shehia hiyo jana, akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya jamii katika Mkoa wa Kaskazini Pemba


No comments: