Saturday, April 28, 2012

HATIMAE MKATABA WA DARAJA LA MBUTU WASAINIWA RASMI, IFM WAADHIMISHA SIKU YA TAALUMA YA CHUO HICHO JIJINI DAR LEO.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Injinia Patrick Mfugale (aliekaa kushoto) na Mwenyekiti Mtendaji wa mradi wa Ujenzi wa daraja la Mbutu Injinia Stephen Makigo wakisaini mkataba rasmi wa Ujenzi wa daraja hilo, ambapo makampuni 13 ya kizalendo yamepewa mradi huo utakaochukua miezi 18 hadi kukamilika, wanaoshuhudia nyuma (mwenye tai) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Injinia Dk. John Ndunguru kushoto kwake ni mwenyekiti wa CRB Injinia Consolata Ngimbwa wengine ni wawakilishi wa makampuni yanayojenga daraja hilo.


Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Injinia Patrick Mfugale (kushoto) na Mwenyekiti Mtendaji wa mradi wa Ujenzi wa daraja la Mbutu Injinia Stephen Makigo, wakibadilishana mafaili mara baada ya kusaini mkataba rasmi wa ujenzi wa daraja hilo jijini Dar es Salaam jana, mradi huo utakamilika baada ya miezi 18

 Wanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha IFM wakiwa kwenye mavazi rasmi ya kazi wakati wa maadhimisho ya Taaluma ya Chuo hicho ambayo huwakutanusha na wataalamu na wadau wa huduma za kifedha kwenye maonyesho yanayofanyka kwenye viwanja vya Makumbusho jirani na Chuo hicho Chini ya Udhamini wa kampuni ya Tigo.
 Hawa ni wataalam wa masuala ya bima wa chuo hicho. Tigo ambao ndio wadhamini wakuu wa maonyesho hayo walishiriki kikamilifu kwa kuweka mabanda yao.
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Cha Usimamizi wa Fedha IFM Charles Nyoni, akikata utepe kuzindua maonyesho ya Siku ya Taaluma kwa chuo hicho kwenye viwanja vya Makumbusho kuu ya taifa jijini Dar es Salaam jana ambayo huwakutanisha wadau wa taasisi za kifedha na wanachuo ilikuona wanvyofanya masomo yao kwa vitendo, wapili kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Prof.Daniel Mjema.

 Mabanda ya tigo nayo yalifurika wateja kupata huduma za papo kwa papo
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Cha Usimamizi wa Fedha IFM Charles Nyoni, akitembelea maonyesho ya Siku ya Taaluma kwa chuo hicho kwenye viwanja vya Makumbusho kuu ya taifa jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuyazindua mapnyesho ambayo huwakutanisha wadau wa taasisi za kifedha na wanachuo ilikuona wanvyofanya masomo yao kwa vitendo, kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof.Daniel Mjema.

No comments: