Wednesday, April 4, 2012

JENGO REFU KARIBU NA IKULU KAMATI YA BUNGE YATAKA MAELEZO

 Jengbo hili refu lililopo Mkabala na Hospitali ya Ocean Roazd jijini Dar es Salaam, limekuwa likizua maneno kadhaa kutokana na kujengwa mita chache kutoka Ikulu. Wanahabari na baadhi ya Wabunge walihoji nyakati mbalimbali juu ya uhalali wa kuwepo kwake hapo kwa madai linahatarisha usalama wa Ikulu.
 Linavyoonekana kwa kwa upana wake.
 Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC) John Cheyo (kushoto) akiongozwa na Kaimu Mteda Mkuu wa wakala wa Majengo (TBA) Injini Elius Mwakalinga (katikati) na Meneja wa Vifaa Phares Tarimo wakati kamati hiyo ilipokwenda kukagua mradi wa ujenzi wa ghorofa refu lililopo karibu na Hospitali ya Oshen Road ambalo tba ni mshirika wa ujenzi huo     

WAKALA wa Majengo nchini ambao ni Washirika wa Ujenzi wa Jengo hilo kama sehemu ya miradi yake ya kibiashara ili iweze kujiendesha ilitoa ufafanuzi juu ya kujengwa kwa jengo hilo.


Wajumbe wakamati hiyo walihoji juu ya kujengwa kwa jengo hilo kwenye eneo nyeti lakini hatga hivyo majibu yake yalikua ni rahsi kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Injinia Elius Mwakalinga ambapo alisema kabla Ujenzi huo kufanyika walifuatgilia kwa mamlaka mbalimbali za Serikali kama kunasheria yeyote itavunjwa kama watgashiriki kwenye ujenzi huo na kukuta hakuna kosa lolote kisheria linalozuia kujenga majengo eneo hilo ila ni mawazo ya watu tu tu na hisia ndizo zilizotawala yakwamba haparuhusiwi kujengwa majengo marefu.


Kutokana na majibu hayo kamati iliridhika na kuamua kufanya ziara ya kulikagua jengo hilo.

No comments: