Sunday, April 8, 2012

JK AWAFARIJI NDUGU WA KANUMBA.


JK ALONGA KWENYE MAOMBOLEZO YA KANUMBA

RAIS Jakaya kikwete amewahimiza wasanii  kukaa chini nakutekeleza waliyokubaliana Dodoma ali aweze kutekeleza ahadi ya kuwapa pesa kwaajili ya mipango hiyo waliokubaliana.

Rais aliyasema hayo muda mfupi tu baada ya kwenda kutoa mkono wa pole kwa nduugu jamaa na marafiki wa msanii maarufu nchini Steven Kanumba Sinza Jijini Dar es Salaam.
Aidha Rais alisema anasikitishwa sana kuona wasainiii wanakua na kipatgo cha chini na wasambazaji ndio wanao faidika kwa kiasi kikubwa.

"Nakumbuka ahadi yangu kwenu ya pale tulipokutana Dodoma lakini nawaomba katekelezeni kwanza yale tuliyokubaliana then kazi yangu ni kuwapa pesa tu na ppesa zipo," alisema Rais.

Kuhusu kifo cha Steven Kanumba Rais alisema mungu hupanga kila kitu kwa utaratibu anaoujua yeye hivyo hata kifo hivyo hivyo hakitokei ila kuna sababu, mwengine huumwa na nyoka, mwengina hulala tu halafu asiamke, mwengine hugongwa na gari basi alimradi mungu anavyo taka mwenyewe.

"Nawapa pole sana wasanii wote ndugu jamaa na marafiki msiba ni wetu sote alikua kijana mdogo sana ambaye angeweza kufanya mambo mengi kaama angeendelea kuwepo lakini mapenzi yake mungu ndo hivyo tena hatunae.

Kazi zake zilitambulika sana hasa Afrika kama vile Kongo Kenya na hata Rwanda na Burundi." alisema JK.

No comments: