Friday, April 13, 2012

KAMA KAWAIDA JIJI LA MARAHA NA KARAHA.

 Wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha IFM wakijisomea kando ya Bahari ya Hindi na kuniacha na maswali mengi kichwani, moja inawezekani hali ya hewa ya joto jijini Dar ndiyo sababu kuu ya kwenda eneo hilo kujisomea.

Pili inawezekana mahali pakujisomea karibu na chuo hamna! na kama ingekuwa ndiyo jibu basi ningeishawishi serikali kuliboresha eneo hilo likawa zuri zaidi kwa kujisomea wanafunzi wa kada mbalimbali.

Nikaamua kufanya uchunguzi mdogo tu nikagundua sababu ya kwenda eneo hilo, nilimuuliza mwanafunzi mmoja Anko vipi mbona bize ndugu yangu unaelekea wapi? Akanijibu E banae Anko bana siunaona washkaji kibao hapa tuna pepa mwanangu ndomana unaona washkaji wanataharuki hapa.
Nikapata jibu nikasema ama kweli bongo ni zaidi ya vile tunavyo ifahamu kwa sababu inaonekana watu tunasomea mitihani hadi leo hiii, badala ya kusoma tuelewe. Nilitghibitisha kauli ya mwanafunzi yule baada kukutana na misururu ya wanafunzi wakijisomea kwenye kuta za bustani zinazotazamana na Makumbusho ya Taifa.
 Hali ya Mto Msimbazi eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam inavyoonekana kwa sasa baada ya mvua chacha iliyonyesha je miundombinu yetu inakidhi mahitaji kwa mvua ya masika tunayoitarajia?

 Hapa ni Eneo la Makutano ya Barabara za Mandela na Nyerere TAZARA jijini Dar es Salaam pakiwa pamejazana maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.
Eneo hili la jangwani ndipo panapotarajiwa kujengwa kituo cha mabasi yaendayo kwa kasi pakiwa pamejaa maji ya mvua baada ya kuandaliwa kwa kuchongwa na greda hivi karibuni. Maji ya mvua ambayo hadi sasa yapo yameharibu mifumo ya vipimo yote.

No comments: