Thursday, April 5, 2012

LEMA AVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.

Taarifa kutoka jijini Arusha zinasema uamuzi huo umefikiwa leo asubuhi Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo. 


Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).


Lema katika Uchaguzi huo alikuwa akichuana vikali na Mgombea wa CCM, Dk. Batilda Salha Buruiani ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya.

Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cham hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.

Pia habari za ndani ya Chama cha Chadema zinasema kuwa tayari Chama hicho kilisha soma alama za nyakati mapema katika kesi hiyo miezi kadhaa nyuma na kujipanga endapo mbunge huyo atavuliwa wadhifa wake nani kimsimamishe kutetea kiti hicho.

Habari hizo zinadai kuwa Chadema kimepanga kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chama hicho na Mgombea Urais wa 2010, Dk. Wilbroad Silaa kutetea kiti hicho.
Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa  wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.

Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5 kujitetea.

Habari kwa hisani ya Father Kidevu Blog.                                                      SOMA MAGAZETI YA LEO


  


 KUTOKA ZANZIBAR, DK. SHEIN AWAAPISHAMAWAZIRIWAPYA                                     
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Ramadhan Abdalla Shaaban,kuwa Waziri wa Ardhi.Makaazi,Maji na Nishati,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana,kabla Shaaban,alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Ali Juma Shamuhuna,kuwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali, katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
jana,kabla Shamuhuna, alikuwa Waziri wa Ardhi, Makaazi Maji na Nishati

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Suleiman Othman Nyanga,kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar, kabla Nyanga, alikuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri
asiyekuwa na Wizara Maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Mansour Yussuf Himid,kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Said Ali Mbarouk kuwa Waziri wa Habari,Utmaduni,Utalii na Michezo, katika hafla iliyofanyika Ikulu
Mjini Zanzibar, kabla Said,alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Abdilah Jihad Hassan,kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi,jana Ikulu Mjini Zanzibar,kabla Jihad alikuwa Waziri
wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Bw Sheha Mohamed Sheha,kuwa Mshauri wa Rais-Pemba,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri aliowaapisha waliosimama,hafla hiyo ilifanyika jana Ikulu Mjini Zanzibar,wengine Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif,(kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kulia).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Lorcan Fullam, aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na mgeni wake Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Lorcan Fullam, aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga
Rais, baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.

Kwaheri ya kuonana.

PICHA ZOTE KWA HISANI YA IKULU ZANZIBAR

No comments: