Tuesday, April 10, 2012

MWISHO WA KANUMBA HAPA DUNIANI NI LEO, ANGALIA MATUKIO YOOTE YALEO.

 KALALE SALAMA STEVEN CHARLES KANUMBA.
 Mama huyu akilia kwa uchungu baada ya kuliona Jeneza lenye mwili wa Kanumba si mama mzazi wa Kanumba na wala si ndugu ila ameshindwa kujizuia.
 Kikundi Cha Kwaya alichokuwa akikiimbia Kanumba walimkumbuka kwa kumuimbia nyimbo alizozitunga wakati wa uhai wake.
 Wema Abraham Sepetu akiwa haamini kinachoendelea kwenye viwanja vya Leaders Club wakati aliyekuwa mpenzi wake wa mwanzo kabisa marehemu Steven Charles Kanumba akiagwa na mamia ya wananchi.
 Mcheza filam maarufu hapa nchini Anti Ezedkiel, akifuta machozi kuona Safari ya mwisho ya Kanumba.
Watoto ambao alifanyanao Filam Marehemu Steven Kanumba, wakiwa katika mavazi rasmi wakiwasili kwenye viwanja vya Leaders jana. Filamu alizocheza na watoto hao ni pamoja na This is it, Anko JJ and Big Dady.
 Mama mzazi wa Steven Kanumba akiwapungia mikono waombolezaji waliofika kuaga mwili wa mwanawe.
 Hapa wanafamilia wakifuatilia ibada zilizokuwa zikiendelea.
 Walikuwepo waliolia na kujifuta machozi kwa kunawa maji.
 Na hili ndilo Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Steven Kanumba
 Swahiba wa marehem Kanumba Dk.Chei Katikati, JB kushoto, Rey kulia na wengine, wakiliweka sawa jeneza ka Kanumba.
 Askari huyu unaweza kusema alipata kitu cha Arusha au cha Msumbiji maana zilimtoka bakora kwelikweli akiwakung'uta waombolezaji wenye fujo na viherehere, mbali na jua lililokuwa likiwapiga lakini nyongeza yao ilikuwa ni bakora za askari huyu dahhhhhhh.
 Idadi ya watu walioanguka hakuweza kupatikana lakini nilioshuhudiwa binafsi hawapungui hamsini na watano huyu akiwa mmoja wao.
 Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilali na mke wake wakiaga mwili huo.
 Mama Salma naye akimuaga kanumba akishindikizwa na Waziri wa Habari Utamaduni na Maendeleo ya michezo Emmanuel Nchimbi, akifuatiwa na Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe.
 Waziri wa Aridhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini mama Anna Tibaijuka ambae alishiriki kwenye maombolezo hayo. Waziri wa Habari Utamaduni na Maendeleo ya Michezo Emmanuel Nchimbi akitoa salaam za Serikali na rambirambi ya Tsh10Millioni.
 Wakazi wa jiji la Dar es Salaam walivyojitokeza kwa wingi kwenye kuaga mwili huo.

 Wanafamilia ya Steven Kanumba.
 Jeneza likiondolewa Leaders Club kwa shida huku gari lililobeba likiwa limesongwa na watu hata kushindwa kutembea.

 Huyu ni miongoni mwa watu wengi waliopoteza fahamu na kuzirai.


 Kundi la watu waliozimika ghafla wakiwa wamekusanywa pamoja ili kurejesha fahamu zao na kupatiwa huduma ya kwanza.
 Wasichana wa Red Cross walifanya kazi ya ziada.
 Likifunuliwa kwa mara ya kwanza watu wachache tu ndio waliopata fursa ya kuona kutokana na msongamano.
 Mama Salma ni miongoni mwa watu wa chache waliopata fursa ya kuona mwili wa marehemu.
 Safari ilianza kama hivi na hii ni barabara ya kutoka Leaders Club kuelekea kwenye makaburi ya Kinondoni.

 Eneo la Makaburini vijana walipanda juu kushuhudia kinachoendelea.


 Wazee wa kazi nao wakatiatimu kurekebisha mambo kwani wahuni nao walitumia fursa hii kutimiza uhuni wao.
Na hapa ndio anahitimisha safari yake hapa dunia.

No comments: