Saturday, April 7, 2012

NINI KILITOKEA HADI KANUMBA AKAPOTEZA MAISHA

TAARIFA za tukio zima nilizonazo baada ya kuhangaika tangu saa 11:30 alfajiri hadi sasa kwa kuanzia kule Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kwamba Kanumba alikwaruzana na rafikiyake wa Kike ambaye ni Elizabeth Michael (Lulu) Pichani.
Mikwaruzano hiyo ambayo ilianza majira ya saa saba za usiku iliendelea wakaamua kujifungia chumbani ambako walikua wakirushiana maneno ambayo hata hivyo kwa mujibu wa mdogo wa marehemu hakuwa tayari kuielezea kikamilifu.

Baada ya hapo Lulu alitoka Chumbani na kumwabia mdogowake Kanumba kuwa Kanumba ameanguka, baada ya kwenda akakuta haliyake ni mbaya akaamua kumpigia simu daktari wake kanumba.

"Nilivyo mpigia daktari wake akiniambia sina usafiri saivi, basi mimi nikachukua gari nikamfuata, alipofika daktari wake akampima akasema muwaishe Muhimbili saivi," alisema

Hata hivyo alisema alionekana akiwa tayari ameshafariki kabla hata hajafikishwa Muhimbili.

POLISI
KAMANDA wa polisi wa Wilaya ya Kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema wanamshikilia rafiki wa kike wa Muigizaji huyo ambae yupo kituo cha Polisi cha Osterbay.
Kamanda Kenyela alisema bado wanaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo na mara upelelezi utakapo kamilika watatoa taarifa kaili.

MASHUHUDA


Watu waliowahi kufika nyumbani kwa Kanumba waliona polisi wakifungua chumba chake na kutoka na Chupa ya Pombe aina ya Jack Daniel ikiwa na pombe kama robo imebaki, glasi ikiwa na kiasi cha pombe kidogo pamoja na Panga pichani.

Hata hivyo wanandugu pamoja na kamati nzima ya mazishi ikiongozwa kwa kiasi kikubwa na wasanii pamoja na watu wa karibu wa kanumba wanasema taarifa za namna ya kifo kilivyotokea kwa jeshi la polisi hivyo kwa sasa familia.


ENDELEA KUFUATILIA TAARIFA ZAIDI.


No comments: