Tuesday, April 17, 2012

SHULE IMEJENGWA TANGU 1977 LAKINI HADI LEO INA MADARASA MANNE TU!


                          
                                     
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibamba iliyopo Eneo la Mwanambaya Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani wakiwa wamekaa chini wakisubiri kukabidhiwa madarasa yao pamoja na madawati ikiwa ni msaada wa kampuni ya Songas.

NIVIGUMU sana kuweza kuamini hili lakini ndivyo ukweli ulivyo na ni bora tuseme kwakua kwa kufanya hivyo ndio tunatimiza wajibu wetu. Shule ya Msingi Kibamba ipo umbali wa wastani wa Kilometa 40 kutoka jijini Dar es Salaam
kama unaelekea mikoa ya kusini kwenye Kitongoji cha Mwanambaya ambako kwenye ziara yangu niligundua sehemu ya uozo kwenye nchi yetu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo anasema Shule hiyo imejengwa tangu 1977, lakini hadi leo hii ina madarasa manne tu tena idadi hiyo ni baada ya kupata msaada wa kujengewa madarasa mawili na kampuni ya Songas.
Msaada huo wenye gharama wa takriban Tsh20Millioni ulijumuisha pamoja na madawati hamsini na ofisi ya waalimu moja.
Shule hiyo yenye idadi ya Wanafunzi 400 inatatizo hilo la madarasa yakusomea kwani kiwango hicho cha wanafunzi hakiendani kabisa na mahitaji kwani ikumbukwe kuwa kuna wanaosoma kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.
Shule hiyo haina vitabu kabisa vilivyopo ni vichache kabisa na vimechakaa kutokana na kusomea nnje ambako hupigwa na jua pamoja na mvua jambo ambalo nikawaida kwa shule hiyo kwa miaka mingi.
Nilipo muuliza Kaimu Afisa elimu wa Wilaya ya Mkuranga Teddy Bagolele, alisema bajeti ya halmashauri ya Wilaya hiyo ni ndogo na miradi hiyo ya shule iko mingi kwa hiyo tegemeo lao limebaki kwa wahisani tu kama hao waliojitokeza. Kwa kuangalia mandhari ya eneo lililopo shule hiyo na wazazi waliohudhuria kwenye hafla ya makabidhiano hayo inaonyesha kabisa wazazi wao kuwa wamechoka na hautatamani kuwashawishi kuchanga pesa hata kidogo labda nguvu kazi inaweza ikawa ndo mchango wao.

 Tunasikiliza.
 Afisa Uhusiano na Maendeleo ya Jamii wa Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Songas akizungumza na waandishi, Wazazi wa wanafunzi na wanafunzi wenyewe mara baada ya kukabidhi msaada huo.
 Watoto wa masikini wa Mkuranga wakifurahia angalau Songas wamewakumbuka kwa madawati na madarsa, wakatoa zawadi ya wimbo kwa songas.
 Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Teddy Bagolele akikata utepe kuzindua jengo lenye madarasa mawili na ofisi moja kwnye shule hiyo na kufanya idadi ya madarasa kwenye shule hiyo kuwa manne, kulia ni Afisa Uhusiano wa Maendeleo ya jamii wa kampuni ya Songas Nicodemas Chipakapaka.
Sehemu ya jengo la madarsa mawili na ofisi ya walimu.

No comments: