Wednesday, April 18, 2012

WABUNGE WAICHANA LIVE SERIKALI

Mbunge wa Nkasi Ally Mohamed Kessy, aliyeitaka Serikali kuwanyonga watendaji wanaofuja fedha za Umma.
 Mbunge wa Kigoma Mjini Peter Selukamba amewataka wabunge wa CCM kukaa chemba kuwaondoa Mawaziri wazembe
 Mkulima wa Tanzania anatamani awe angalau kama Mzee huyu.

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameichana chana Serikali, kwa kufanya uzembe wa kutochukua hatgua za kisheria kwa watendaji wabovu.

Wabunge hao waliongea kwa hasira na kufikia kutoa manene makali ambayo kwa kiasi kikubwa yataleta athari kwa jamii hususan chama cha mapinduzi.

Wakijadili ripoti za kamati za ukaguzi wa Fedha za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na za Nashirika ya Umma. Taarifa za kamati hizo ziliwachefua wabunge na kuibua hasira zao na kumtaka Rais Kikwete aache upole na achukue hatua.

Kilichokera zaidi wabunge ni matumizi mabaya ya fedha za Serikali kwa mashirika ya Umma,Serikali Kuu na Serikali za Mitaa hali iliyosababisha hasara ya mabilioni ya Shilingi.

Mbunge wa Nkasi Ally Mohamed Kessy alipendekeza kupelekwa kwa mswaada maalum bungeni wa kutunga sheria ya kuwanyonga Viongozi wanao kula fedha za umma.

Haifurahishi na wala haipendezi kuona watanzania wanakufa na njaa, wanakosa huduma za afya barabara mbovu halafu watu wanatanua kwa matumizi ya ajabu kwa pesa za umm.


"Ikiwezekana hawa watu hata kesho wanyongwe kwani wanajulikana hii ni nchi gani hii," Alisema Kessy.

Mbunge wa Mwibara,(CCM), Kangi Lugora, alisema kunawakati alishikwa na hasira hadi kufikia hatua ya kutaka kumpiga ngumi mmoja wa watumishi wa Serikali kupitia Taasisi moja, baada ya kuwafungisha safari hadi nnje ya nchi kwenda kukagua ofisi hewa ambayo haikuwepo kabisa na kurudi nchini bila faida yeyote.Aidha wabunge hao walilalamikia kitendo cha Mawaziri wa husika kutokuwepo kwenye mjadala huo hali wakijua kuwa ni jambo muhimu sana kwa nchi badalayake hawaonekani.


Mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba aliwataka wabunge wa CCM kuisaidia Serikali, Rais Pamoja na Wananchi kwa kuwaondoa baadhi ya mawaziri ambao wanaonekana wazembe.


Sisi wabunge tusilalamike tutumie kanuni tu tutawaondoa mawaziri wabovu mmoja baada ya mwengine lakini tukisema tumsubiri Raisi hatamuondoa hata mmoja, wabunge wa CCM kesho tukae chemba hii ni aibu kwa Serikali yetu.

TUTAENDELEA KUWALETEA TAARIFA KEM KEM ZA MJENGONI.

No comments: