Tuesday, April 17, 2012

WABUNGE WAPYA WA EAC WAPATIKANA


Miongoni mwa waliochaguliwa kuwa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki ni pamoja na Shyrose Bhanji pichani akisalimiana  na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
 Aliyekuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kawe Angela Kizigha ameukwaa Ubunge wa Jumuia ya Afrika Mashariki kwenye uchaguzi uliomalizika hivi punde.
 Makongoro Nyerere (mtoto wa hayati baba wataifa) nae amechaguliwa kuwa mbunge wa Jumuiya hiyo.
 Hapa Makongoro akiwa na mama Fatma Karume alipomtembelea Nyumbani kwake Butiama.

                                          
Aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Adam Kimbisa nae amechaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Dada wa Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi James Mbatia,Ms Perpetua Nderakindo Kessy, nae amechaguliwa kuwa mbunge wa bunge hilo la Afrika Mashariki.

WENGINE ni Abdallah Mwinyi CCM, Twaha Issa Taslima, Bernad Muranya CCM  na Mariyam Ussy Yahya CCM.

No comments: