Wednesday, April 4, 2012

WANAFUNZI WA IMTU WAISHUKURU SERIKALI KWA KUTATUA MGOGORO WAO.

 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Cha Afya cha IMTU (IMTUSO) Cha jijini Dar es Salaam Mr. Chacha, akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kumalizika kwa mvutano kati ya wanafunzi, Chuo na Serikali uliodumu kwa miezi 7 na kukosa kuingia darasani kwa kipindi chote baada ya kutekelezwa kwa madai yao kwa asilimia 90.
 Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi IMTU (IMTUSO) Mr.Msafiri akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari.

 
WANAFUNZI wa Chuo Cha Afya Cha IMTU Cha jijini Dar es Salaam leo wameishukuru Serikali na wadau wote waliojitolea kwa hali na mali katika kuwasaidia kutatua mgogoro kati ya wanafunzi, Chuo na Serikali kwa upande mwengine uliodumu kwa zaidi ya miezi saba hali iliyowakosesha masomo kwa muda wote huo.


Aki
zungumza mbele ya Waandishi wa habari Rais wa Serikali hiyo Mr Chacha alisema ni vema ieleweke kuwa mgogoro huo ndio mgogoro pekee miongoni mwa migogoro ya vyuo uliochukua muda mrefu zaidi kutatuliwa. Kutgokana na hali hiyo kuna mambo mengi wamejifunza kama wanafunzi lakini pia na wadau wengine wa elimu ikiwemo Wizara husika, bodi ya mikopo ya wanafunzi na hata TCU.


Aidha wanafunzi hao walidai kuwa madai yao yametekelezwa kwa asilimia tisiini hali iliyoleta utulivu kwa wanafunzi.


"Yametekelezwa mengi kwa mfano tulikua tunalalamikia ulipaji wa ada kwa mfumo wa dola lakini sasa tunalipa kwa Shilingi, tulikuwa tunalalamikia ada kubwa ya $7,000 lakini sasa tunalipa Tsh6.2Millioni"

Kutokana na mazingira hayo wanafunzi hao wametoa kauli ya kuboreshwa kwa mazingira ya elimu ya chuo hicho ambayo kimsingi yanatokana na mgogoro huo ambapo waliwataka watanzania kujenga imani na chuo hicho kwa madai kuwa mgogoro huo sasa umeisha.

"Hakuna taasisi isiyo na migogoro kabisa sujala la msingi ni kukaa pamoja na kuzungumza" Walifafanua.

MWISHONo comments: