Wednesday, April 18, 2012

YALIYOJIRI JIJINI DAR LEO, Maonesho ya Vyuo Vikuu, Waathirika wa mafuriko Wapata Viwanja, Mkurabita Watoa Somo.

 Kjana huyu mkazi wa jiji la Dar es Salaam alinaswa na Kamera ya blog hii eneo la Magomeni Mapipa akielekea mjini na usafiri wake wa baiskeli ya gurudumu moja.
 Wakazi wa eneo la Mtaa wa Suna Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam ambao walikumbwa na mafuriko wakimsikiliza Mwenyekiti wao wakati akisoma majina ya watu waliopatiwa viwanja eneo la Mabwepande.

 Mkazi wa jiji la Dar es Salaam akisaini kitabu wakati alipohudhulria maonesho ya Vyuo Vikuu jijini Dar es Salaam. Na hili ni banda la Chuo Kikuu cha Elimu Zanzibar, kulia ni Muhudumu wa
 Banda la Chuo Kikuu cha TUMAINI
 Banda la Taasisi ya Elimu Tanzania.

 Mtangazaji wa PPR Pascal Mayala, akimuhoji Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo mara baada ya kufungua Kikao cha Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kushoto ni Mratibu wa Mpango huo, Seraphia Mgembe, akifuatiwa na Japhet Werema Meneja wa Urasimishaji Mijini na wapili kulia ni Stephen Rusibamayila. Kukao hicho kilihusisha Viongozi wa Mpango huo na Waandishi wa Habari.
Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo, akiwahutubia waandishi wa habari ambao walihudhuria kwenye mkutano huo wa kuwaelimisha mafanikio na changamoto za utekelezaji wa majukumu ya mpango huo na kujadili hatua za kusonga mbele.
MRATIBU WA MPANGO WA MKURABITA SERAPHIA MGEMBE.

No comments: