Saturday, April 7, 2012

YALIYOJIRI JIONI NYUMBANI KWA KANUMBA

 Wapenzi na mashabiki wa Steven Kanumba wakiwa wamefunga njia kabisa kutaka kushuhudia kila kinachoendelea nyumbani hapo kama walivyokutwa na blogger jioni hii.
 Dada wa Marehemu Stevene Kanumba (katikati) Abela Kajumlo, akifarijiwa na ndugu na jamaa waliofika kwenye msiba huo.
 Mmoja wa wasanii wakongwe waliowahi kuigiza na Steven Kanumba, akilia kwa hisia kali kutokana na ukaribu waliokuwanao wasanii hao.
 Mbunge wa Viti Maalu CCM Vicky Kamata,akisaini kitabu cha maombolezo.
 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Mr.II Sugu) akiwasili msibani.
 Msanii wa muziki wa kizazi Kipya Shelta naye alikuwepo na hapa akiwasili msibani hapo.
 Rais wa FM Academia Nyosh Elsadat naye alikuwepo kwenye maombolezo hayo na hapa akiwasili.
 Mbunge wa Manyoni Mh.Alhaji Juma Suleiman Mkamia akisalimiana na watu mbalimbali.
 Mandhari ya eneo ilipo nyumba inavyoonekana kwa juu huku mashabiki wa kanumba wakiwa kwenye kuta za fensi na paa za nyumba kutaka kushuhudia kinachoendelea.
 Ulinzi uliimarisha na hapa ni mlangoni vijana wakitaka kuingia ndani wakati kukiwa kumejaa.

No comments: