Saturday, April 7, 2012

YANAYO ENDELEA BAADA YA KIFO CHA KANUMBA.

PICHA YA MAREHEMU STIVEN KANUMBA PEMBENI YAKE KUKIWA NA MSHUMAA IMEWEKWA UKUMBINI NYUMBANI ALIPOKUWA AKIISHI SINZA VATICAN.
 Baadhi ya watu wa karibu na msanii huyo wakiwasili nyumbani kwa msanii huyo leo mapema asbuhi.
Wasanii waliowahi kufika mapema leo asubuhi nyumbani kwa kanumba wakiwa wamekaa kwenye mikeka kabla hapajafungwa matent wala viti vikiwa havijaletwa bado. Huzuni na vilio ni kitu kilichokuwa kimejiri kwenye eneo hilo.
 Mwanamitindo Mashuhuri nchini Tanzania Hapiness Magese, akiwasili nyumbani hapo huku akiwa na huzuni.
Wema Sepetu zao la Msanii Kanumba alikua hajiwezi kabisa akitokwa na machozi muda wote nyumbani hapo.
Kwauujumla idadi kubwa ya watu waliofika muda wa asubuhi ni wasanii wenzake majirani na mashabiki wake wa eneo la Sinza.
Mawasiliano yalikuwa ni muhimu ilikutoa taarifa na kuwaelekeza watu eneo husika, huyu ni mchekeshaji maarufu kwa jina la Mboto.

Vijana mbalimbali walijitokeza kusaidia kazi, hapa vijana hawa wakibeba choo cha kuhamisha ikiwa ni maandalizi ya kuweka huduma muhimu kwa watu watakao fika nyumbani hapo.

ENDELEA KUFUATILIA TAARIFA HIZI ZITAKUJIA KILA WKATAI.

No comments: