Friday, April 20, 2012

ZITTO KABWE APIGWA MWELEKA NA KANUNI ZA BUNGE, Hoja yake ya kumtimua Pinda yapigwa chini.

Taarifa za hivi punde kutoka Bungeni Mjini Dodoma zinasema Kusudio la mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, lakutaka kumuondoa Waziri Mkuu Mizedngo Pinda kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae limepigwa chini na Spika Makinda.


Akisoma kanuni Mh. Makinda alisema kwa mujibu wa kanuni na katiba ya nchi kusudio la kutaka kumuondoa Waziri Mkuu kwa kupiga kura ya kutokuwa na Imani taarifa ya maandishi inapaswa kuwasilishwa kwake siku 14 kabla ya siku husika.


Kwakuwa ofisi yake haijapata taarifa ya maandishi zoezi hilo litakuwa batili, kwasababu kikao hicho cha bunge kinafungwa juma tatu hakutakuwa na uwezekano wa zoezi hilo kukamilika.


Awali Mbunge wa Bumbuli January Makamab, aliomba muongozo wa Spika kuhusu jambo hilo ndipo spika makinda akasimama kutoa ufafanuzi huo juhudi za kumpata Zitto Kabwa zinaendelea punde akitoka mjengoni.

No comments: