Wednesday, May 2, 2012

DAKTARI SHEIN ZIARANI KASKAZINI UNGUJA.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Pembe Juma Pembe,(kulia) wakati alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni akiwa  katika ziara ya Mkoa huo iliyoanza leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, (wa tatu kushoto) akipata taarifa ya utekelezaji wa kazi za  Mkoa wa Kaskazini Unguja,iliyosomwa na Maalim Maulid Nafasi Juma, katika  ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya  miradi mbali mbali ya kijamii katika Mkoa huo.

Picha na Ramadhan Othman Ikulu Zanzibar

No comments: