Thursday, May 3, 2012

DK.SHEIN KWENYE HARAKATI ZA MAENDELEO KASKAZINI UNGUJA.

Wanafunzi wa Skuli ya Kitope wakimsikiliza Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,wakati alipozungumza na wazee katika sherehe za uzinduzi wa Madarasa mapya katika Skuli hiyo, baada ya uzinduzi, alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za jamii katika wilaya ya Kaskazini.
Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na viongozi wa Chama Wilaya ya Kaskazini A,alipofika kuweka  jiwe la msingi Tawi la CCM -Kibuyuni Jimbo la Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uwekaji wa jiwe la msingi Tawi la CCM -Kibuyuni Jimbo la Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, alipofanya ziara ya kuimarisha Chama katika Mkoa huo.

Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Skuli  ya Maandalizi ya Fujoni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia    Wananchi wa Bwekunduni baada kuizindua barabara ya kifusi katika shehia hiyo, alikuwa kwenye

ziara ya Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna, akizungumza na wananchi na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, ili awasalimie Wananchi wa Matemwe Kigomani na kutoa nasaha zake wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi madarasa mapya katika Shehia hiyo,alipokuwa katika ziara ya  kuangalia maendeleo ya miradi mbali mbali ya kijamii katika Wilaya ya Kaskazin.

No comments: