Tuesday, May 8, 2012

DK.SHEIN ZIARA ZINAENDELEA SASA NI MKOA WA KUSINI UNGUJA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili, Affani Othman Maalin,kuhusu matumizi ya daraja la mikoko wakati alipotembelea maendeleo ya wakulima wa Jozani wilaya ya kusini, alipokuwa katika ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya kilimo katika Mkoa wa Kusini Unguja jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiangalia mashine za uchunguzi wa maradhi mbali mbali ya Binadamu katika kituo cha Afya cha mwera Ponge baada ya kuweka jiwe la msingi jana alipokuwa katika ziara ya kuona maendeleo ya miradi mbali mbali katika Mkoa wa kusini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha Afya cha Mwera Pongwe jana,akiwa katika ziara ya
Wilaya ya Kati Unguja kutembelea Maendeleo ya ya Miardi mbali mbali ya kijamii katika Mkoa wa Kusini Unguja.ujenzi huo umefadhiliw na mwekezaji kutoka nchini Italy Dominic Palumbo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim,alipotembelea maandalizi ya
kilimo cha Mpunga wa umwagiliaji huko Bonde la Uzini Wilaya ya Kati Unguja jana.

No comments: