Monday, May 21, 2012

FLAVIANA MATATA ATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUJIOKOLEA MAJINI:


Wakati leo Watanzania wakitimiza miaka 16 tangu kuzama kwa Meli ya MV Bukoba Mwanamitindo wa Kimataifa wa nchini Tanzania Flaviana Matata, ambaye naye alimpoteza mamayake mzazi kwenye ajali hiyo ametoa msaada wa vifaa vya vya kuokolea maisha ya watu katika vyombo vya usafiri wa maji ambavyo vimelengwa maalum kwa Ziwa Viktoria mjini Mwanza. 

Msaada wa vifaa hivyo umeelekezwa katika shirika la kiserikali la usafiri wa maji jijini Mwanza lijulikanalo kama Marine Service Co. Ltd.Flaviana Matata ametoa jumla ya vifaa hivyo 500 (vyombo vya kuokolea maisha ndani ya maji) ikiwa ni kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MvBukoba mnamo May 21 mwaka 1996 ambapo pia alimpoteza mama yake mzazi.

 Kwenye ajali hiyo iliyouwa watu takribani 1,000. Sababu mojawapokubwa iliyofanya watu kupoteza maisha yao siku ya tukio hilo ilikuwaupungufu na ukosefu wa vifaa vya majini kama maboya (Live Vest).


Naamini kwamba, watu waliofariki katika ajali ya meli ya Mv Bukoba wengi walipoteza uhai wao kwa sababu walikosa vifaa vya kujikwamua ndani ya maji, hivyo ndo maana nimeamua leo katika kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba nije kutoa msaada wa vifaa hivi 500’ alieleza Flaviana Matata.

Vilevile akaongeza kuwa ni vyema vyombo vya majini vikawa na utaratibuwa kutoa elimu na maelekezo jinsi ya kutumia maboya endapo kutatokea tatizo kabla ya kuanza kwa safari kama wafanyavyo katika usafiri wa anga.
 

No comments: