Thursday, May 17, 2012

H.BABA AENDELEZA MASHAMBULIZI KANDA YA KASKAZINI. Chini ya Udhamini wa Kampuni ya Tigo.

Msanii  wa Muziki wa kizazi kipya,Hamis Baba maarufu kama H Baba akiwapagawisha mashabiki wake kwenye Kituo cha mabasi wilayani Karatu mkoa wa Arusha katika Bonanza lililoandaliwa na Tigo na kutoa zawadi kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria. Picha na mpigapicha wetu


 H.Baba kazini!

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya,Hamis Baba maarufu kama H Baba(kulia) akiimba na kucheza na watoto waliojitokeza  kwenye Kituo cha mabasi wilayani Karatu mkoa wa Arusha katika Bonanza lililoandaliwa na Tigo na kutoa zawadi kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria. Picha na mpigapicha 


Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

 ‘Pata muda wa maongezi mara mbili na Tigo”

16 Mei, 2012, Dar es Salaam. Kwa mara nyingine kampuni ya Tigo imeonyesha nia ya kutoa huduma bora kwa wateja wa malipo ya kabla kwa kuzindua  promosheni ya “Pata muda wa  maongezi mara mbili na Tigo”

 “Tunafuraha sana kutoa thamani hii ya  fedha kwa wateja wetu” alisema Alice Maro ambaye ni afisa uhusiano wa Tigo. “Promosheni hii ni zawadi nyingine kwa wateja wetu ili kuwawezesha kuendelea kufurahia huduma bora na nafuu kutoka Tigo, kwani tuna lengo la kurahisisha mawasiliano na kufanya maisha yao yawe rahisi na bora” alisema.

Promosheni hii ambayo itadumu kwa siku nne, itawawezesha wateja wa malipo ya kabla watakoongeza salio kupitia Tigo Pesa au Tigo Rusha kupata muda wa maongezi wa ziada. Wateja watapata muda wa maongezi uliolipiwa na dakika za nyongeza kutegemea na kiwango walichoongeza, dakika za ziada zitawawezesha kuwapigia ndugu, jamaa na marafiki wawapendao. Baada ya kuongeza muda wa maongezi, wateja watapata ujumbe wa maandishi kama uthibitisho wa kuanza kutumia muda wa ziada wa maongezi.


Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na  Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.

No comments: