Wednesday, May 23, 2012

JESHI LA POLISI KWA HILI HATUPO PAMOJA.

 Kitendo cha Jeshi la Polisi kuacha eneo hili la Usalama Magomeni likiwa Chafu kwa mrundikano wa magari mabovu wanayoyakamata maeneo mbalimbali hakikubaliki.

Eneo hili binafsi nimewahi kuliandikia mara kadhaa lakini hakuna hatua yeyote inayochukuliwa na Jeshi hilo jambo linalo endelea kuhatarisha afya za watu wa eneo hilo.

Eneo hili maji hutua wakati wa mvua na kusababisha harufu kali, hali inayo lalamikiwa hata na baadhi ya wafanyakai wa karibu na eneo hilo na kudai kuowepo kwa ongezeko la Mbu kutokana na maji taka. Wahusika ondoeni pamba masikioni na Hasa Manispaa ya Kinononi mjue huu ni Sehemu ya Uchafu.

No comments: