Monday, May 21, 2012

KICHANGA CHAOKOLEWA HAI CHOONI,

KICHANGA  CHAOKOLEWA  HAI CHOONI
 
Mwanja Ibadi Lindi
 
KIKOSI cha zimamoto na uokoaji katika manispaa ya Lindi  kwa
kushirikiana na jeshi la polisi wamefanikiwa kuokoa  maisha  ya  mtoto
mchanga wa siku moja aliyekuwa ametumbukizwa choonimara baada ya
kuzaliwa  na  anayesadikiwa kuwa mama ni mama yake  mzazi.

Mtoto huyo wa  kike  wa siku  moja mwenye uzito wa kilo  tatu
aligunduliwa  jana  majira ya  saa  tatu asubuhi kwenye choo cha
shimo kinachotumiwa  na wanafunzi  wa shule  ya  msingi  Mtanda.

Kichanga  hicho kiligunduliwa na wanafunzi wa darasa  la sita wa shule
hiyo ya msingi Mtanda Yasini Selemani wakati alipokwenda  chooni huku
kujisaidia  na kusikia sauti ndogo kama kitoto cha mbuzi  ndani ya
shimo  la choo hicho.

Selemani alisema  baada ya  kusikia sauti hiyo alikwenda kutoa
taarifa kwa  walimu wake wa darasa Dancan Kunguluche, aliyekuwa
akisimamia  mitihani yao ya mfano ya mwishoni mwa juma ambaye
alipokwenda alisikia sauti ya mtoto mchanga.

Baada  ya  jitihada  za jeshi la uokoaji  kufanikiwa  kumtoa mtoto
huyo akiwa  hai huku akiwa  amefunikwa  kwa  kanga na kutumbikizwa
kwenye  mfuko  wa Rambo alikimbizwa  hospitali ya Rufaa ya Sokoine
kwa  kutumia  gari ya  wagonjwa la manispaa ya Lindi ambamo alikuwamo
afisa  muuguzi wa  manispaa  Hadija Jamadini.

Aidha  afisa muuguzi huyo alisema kuwa mtoto aliokolewa wakati alikuwa
hajakatwa kitovu na huku akiwa na uchafu  wa mama yake,damu na  ule wa
chooni na  kwamba alilazimika  kuanza  kutoa  huduma  kwa  mtoto huyo
kwa  kumkata kitovu chake na kukitenganisha.
Kwa upande wake kamanda wa polisi Sifueli Shirima, alikiri kuwepo  kwa
tukio ilo  na kueleza  kuwa kwa sasa  mtoto huyo ameifadhiwa
hospitali  ya mkoa  sokoine huku akifanyiwa uchunguzi  wa afya  yake
wakati jeshi la polisi kwa kushirikiana  na  wananchi wameanzisha
msako wa  kutafuta mama aliye husika na kitendo hicho  cha kinyama.
mwishoo

No comments: