Monday, May 21, 2012

MA DC WA MKOA WA LINDI WALIVYO APA.

                                                                      Abdallah Hamisi Ulega (DC,Kilwa),
                                                                      Dkt, Nassoro Ally Hamidi, Lindi.
                                                                   Ephem Mbigi Mmbaga (DC Liwale)

                                                                  Regina Reginal Chonjo (DC Nachingwea)
                                                                   Agnes Elias Hokororo (DC Ruangwa)

 Walivyo apa.

 Mashuhuda.


MKUU wa mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila, amewataka wakuu wa wilaya mkoani humo, kufanya kazi waliyokabidhiwa ikiwemo kuwatumikia wananchi katika maeneo yao kwa kufuata kanunu na maadili kwa kushirikiana na jamii ili kuwaletea maendeleo kutokana na hali duni za wananchi wamkoa wa Lindi wenye raslimali nyingi
 

Wito huo umetolewa na muda mfupi baada ya kuapishwa wakuu wapya wa wilaya za Mkoa wa Lindi ambapo aliwahimiza kufuata kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali zilizowekwa na Serikali, kwani ndio misingi mikuu itakayowasaidia kutekeleza vema majukumu yao ya kila siku katika wilaya zao.
 

Aidha alisisitiza wakuu hao kusimamia na kufuatilia miradi
inayotekelezwa katika wilaya zao,pamoja na kuzingatia fedha
zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wake inalingana thamani halisi
ya fedha inayotolewa (Value for money).
 

Mara baada ya kuapishwa mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdallah Hamisi Ulega alieleza kuwa kwa nafasi yake atatekeleza vema maamuzi ya vikao vya serikali na kusimamia hasa maamuzi ya Kamati ya Ushauri mkoa(RCC)kuhusiana na ununuzi wa zao la ufuta linalozalishwa kwa wingi wilayani kwake.
 

 Nae mkuu wa wilaya ya Nachingwea Regina Reginal Chonjo,Licha ya kushukuru kwa kuteuliwa Mkuu wa wilaya hiyo alihaidi kushirikiana na wananchi wa wilaya hiyo ambao tayari wamemwonyesha njia baada yawananchi hao kujitolea kujenga jingo la ofisi ya mkuu wa wilaya na Halmashauri yao.
 

Wakuu walioapishwa ni Dkt, Nassoro Ally Hamidi,aliyepangiwa wilaya yaLindi, Abdallah Hamisi Ulega (DC,Kilwa),Regina Reginal Chonjo (DCNachingwea), Agnes Elias Hokororo (DC Ruangwa) na Ephem Mbigi Mmbaga (DC Liwale).
 

Picha na Habari toka kwa mdau Abdulaziz Lindi
Mwisho.

No comments: