Thursday, May 24, 2012

MNYIKA AIMWAGA CCM MAHAKAMANI, Mitaa jijini Dar yarindima kwa Shamrashamra polisi walinda maandamano yasiyo na kibali.

Mbunge wa Ubungo John Mnyika akibebwa Juu Juu baada ya kuibuka Mshindi kwenye kesi ya kupinga matokeo ya Ushindi wa Ubunge kwenye Jimbo hilo kutokana na madai ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi na vurugu zilizofanywa na wafuasi wa chama hicho. Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Hawa Ng'umbi alifungua kesi hiyo kupinga matokeo.

Ushabiki Ukizidi Unafanana kabisa na Ulevi Unapozidi lakini kila mtu ana kiasi cha uwezo wa kuzuia hisia zake, Jamaa furaha mpaka moyoni.
Walioumia pia walikuwepo ingawa ilikua furaha, inawezekana afya nayo maana safari ilikua ni ndef na wengine bila kujali afya zao waliingia kundini kwa furaha.
 Ndani ya Mahakama kuu hali ilivyo kuwa.

 Duh Yaani hadi Lugha ya Kiarabu ilitumika kufikisha Ujumbe "KUN FAYA KUN" Maanayake Kuwa na Inakuwa hivyo, Yani Mungu akisema Kuwa basi limekuwa jambo lilelile alilokusudua kuwa.
 Nasisi tumoooooooooooooo
 Mnyika akiwa Jimboni kwake punde baada ya kuwasili.
 Safari hatua Ila tutafika Tuuuuuu Chadeeeemaaaaaaaaaaaaaa Vemaaaaaaaaaaa.
Hapa Mbunge huyo akiwa na wafuasi wake waliomuunga Mkono Tangu Mahakama Kuu mpaka Jimboni.

 Askari wa Kikosi cha FFU wakifuatilia kila hatua ya maandamano yasiyo rasmi yaliyofanywa na wafuasi wa Chadema baada ya Mbunge wa Chama hicho kuibuka mshindi kwenye kesi ya kupinga matokeo ya jimbo hilo.
 'Mpaka tujue mnaishia wapi'
 Hapa wafuasi mzuka umepanda!
 Mitaa yote hadi Ubungo ndivyo walivyokua wakisikika wakiimba.
 Nguvu ya Wazee wa kazi iliongezwa kwa usalama zaidi.
 Wapo walioumia kwa kuanguka.
 Presha zikazidi "Labda mazoezi hajafanya! Hapana imempushi pikipiki! A a a ameanguka, basi kila mmoja alisema lakwake lakini kiukweli jamaa alidondoka na kuishiwa nguvu.
 Ushabiki ni ulevi banaaaaaaaaa
 Hamsikiiiiiii! Piteni Pembeni tutalianzisha! Ohooooooooo!
Askari hawa sikama walikua wakizuia maandamano hapana hapa wakiwaamrisha waandamanaji kupita pembeni ya barabara ili watumiaji wengine wa barabara wasikwazike na tukio hilo.

No comments: