Thursday, May 10, 2012

DK.SHEIN AMALIZA ZIARA KUSINI UNGUJA AKUTANA NA WATENDAJI WA AIZARA YA AFYA.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya, katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar ,(kushoto) Makamu wa Kwanza wa Rais wa ZanzibarMaalim Seif Sharif Hamad. 

Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya wakimsikiliza Dk.Shein.
Baadhi ya  Viongozi na watendaji katika ofisi mbali mbali za Mkoa wa Kusini Unguja,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa na mazungumzo na watendaji hao katika mkutano wa majumuisho ya ziara aliyoifanya katika Mkoa wa Kusini Unguja,mkutano huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu,Wilaya ya  Kati Unguja.
Akiwahutubia wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati) akifuatana na viongozi na kuingia katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu katika mkutano wa  watendaji  wa Ofisi za Serikali Mkoa wa Kusini  Unguja, katika mkutano wa majumuisho uliofanyika Chuoni hapo jana.baada ya kumaliziki kwa ziara  ya Rais katika Mkoa huo.

No comments: