Sunday, May 20, 2012

STAKABADHI GHALANI KWISHNEI KILWA, Madiwani waupiga teke mfumo huo, sasa biashara ni huria wanachi wachekelea.


Moja ya Maeneo ya Mapumziko Pale Kilwa Pakijulikana kama Kimbilio Loge.
BARAZA la madiwani Wilayani Kilwa limepitisha kwa pamoja azimio la kuondoa mfumo wa Stakabadhi ghalani kwenye zao la ufuta na kuruhusu wafanyabiashara na wananchi kuuza na kununua zao hilo nnje ya mfumo huo.
 Baraza hilo limependekeza kuwa kwa yeyote anaetaka kununua zao hilo atalazimika kukata leseni kwa Mkuu wa Wilaya kwa gharama ya Tsh. 200,000.
Mbali na Ushuru huo wafanyabiashara hao watatakiwa pia kulipia ushuru wa tani 50 kwa Halmashauri hiyo ambapo bei kwa Mkulima imependekezwa isiwe chini ya Tsh.1200 kwa kilo.
Aidha katika hatua ya kusisitiza hatua hiyo madiwani hao wamesema endapo RCC kama itapindisha maamuzi hayo Kilwa  madiwani hao watatoa tamko ikiwa ni pamoja na kujiorodhesha na kupiga kura ya kutokuwa na imani na Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Mze Mtopa, na madiwani wote waliunga mkono kwa pamoja maamuzi hayo.


No comments: