Wednesday, May 23, 2012

TAHADHARI YA TANESCO YAPUUZWA JIJINI DAR.

Pamoja na Shirika la Umeme Tanzania Tanesco  kutoa Tahadhari kwa watu waliojenga chini ya nyaya za umeme zenye Msongo Mkubwa wa KV na kuahidi kuanza kubomoa majengo yote hapo kesho lakini hadi leo hii jengo kama hili pichani bado halijabomolewa.

Jengo hili lipo eneo la Bamaga Mwenge jijini humo karibu na Sheli pamoja na kuambiwa abomoe lakini inaonekana kuna ukaidi juu ya amri hiyo kutekelezwa. Shirika hili kwa takribani siku tatu sasa zimepita tangu lianze kutanga kuwa kuanzia kesho litaendesha opereshani ya bomoa bomoa kwa majengo yote yaliyojengwa kwenye maeneo ya Msongo Mkubwa wa Umeme wa Kv.


No comments: