Wednesday, May 23, 2012

TANZIA BWANA ALITO BWANA AMETWAA JINALAKE LITUKUZWE.


TANZIA1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi anasikitika kutangaza Vifo vya aliyekuwa Katibu Muhtasi wa Kitengo cha Uhasibu, Bibi Theresia Mosha kilichotokea nyumbani kwake Kinyerezi  jijini Dar es Salaam tarehe 21/05/2012.
Taratibu za kuuaga mwili wa Marehemu zitafanyika nyumbani kwake Kinyerezi kesho tarehe 24/05/2012 kuanzia saa 4.00 asubuhi na baadae kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Kilema Moshi kwa Mazishi.                                                             Saad Fungafunga
Na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi pichani, Mhandisi Saad Fungafunga kilichotokea alfajiri tarehe 23/05/2012 katika hospital ya TMJ jijini Dar es Salaam.
Mazishi yatafanyika tarehe 24 Mei 2012 saa 7.00 Mchana , nyumbani kwake kipunguni kwa Mkuleba kwenye makaburi ya Kipako, baada ya Salat Adhuhuri.
Watakumbu kwa daima kwa mchango wake katika taifa hili.
Mungu azilaze  roho  za marehemu hawa  mahali pema peponi. Amin.

1 comment:

Anonymous said...

maskini Funga Funga, nilikuwa nikimfahau huyu engeneer, last week nimeenda ofisini kwake nikaambiwa anaumwa, kazi ya Mungu haina makosa