Thursday, May 3, 2012

UNAWAJUA WABUNGE ALIOTEUA JK WAFAHAMU VIZURI.

 Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR Mageuzi James Mbatia ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 Amekuwa na siasa za Kisayansi zaidi kwenye kipindi chote na nimchambuzi wa masuala ya elimu kwa nyakati tofauti anpopata fursa hiyo.
Ni muumini mkubwa wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini akilenga zaidi kwenye muungano utakaoleta tija zaidi kwa pande zote mbili.
 Amekua akihubiri suala la amani kwa taifa la Tanza huku kwa kiasi kikubwa akipinga ujbaguzi wa aina yeyote. Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya Kisiasa Raisi Kikwete hajakosea kumteua ingawa anatoka kwenye chama cha upinzani.
Mbatia amekua akiamini kujenga hoja katika kufanya siasa na siyo masuala mengi kwani kwa kufanya hivyo taifa linaweza kunufaika zaidi kuliko kuwa na taifa la Porojo.
 Sospeter Muhongo ni Professor wa Geolojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ameteuliwa na Rais Kuwa Mbunge kwa mamlaka aliyopewa na katiba ya kuteua wabunge wasiozidi 10, ambapo hadi hivi sasa ameshateua wabunge 6 na kubakisha nafasi 4.Prof. Muhongo ni Mtanzania aliezaliwa Mji wa Musoma.
 Mteule Mwengine wa Rais ni Mama Janet Mbene  yeye ni Mtanzania aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya CCM kwenye bunge la Tisa. Amewahi kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya KCB, sina hakika kama bado anaendelea kuishikilia nafasi hiyo hadi hivi sasa. Mama Mbene pia ni Katgibu Mkuu wa Tanzania Professional Network (TPN) .
Mama Mbene akiwa kwenye moja ya Shughuli za kijamii kwa kuelekeza jicho lake huko wanakuishi wasiojiweza.

No comments: