Saturday, May 12, 2012

WATOTO WANAOUGUA SARATANI MUHIMBILI WAPATA MSAADA.

Mwenyekiti wa kikundi cha Kutumikia Watu Wenyeshida (SAVE THE NEEDY) Cha jijini Dar es Salaa Doreen Makaya, akiwapa sabuni watoto wagonjwa wa Saratani waliolazwa kwenye Wadi ya Tumaini kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 Watoto wakipokea msaada wa nguo kutoka kwa Doreen.

Kikundi cha kutumikia wenye shida 'Save The Needy' kimetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wagonjwa wa saratani waliolazwa kwenye Wadi ya Tumaini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya wanakikundi hao Mwenyekiti wa kikundi hicho Doreen Makaya alisema wametoa msaada huo baada ya kuguswa na hali mbaya za wagonjwa hao mbao wanahitaji kusaidiwa ili na wao waweze kurudi kwenye maisha ya kawaida.

Msaada huo ni wa Nguo za mitumba, Sabuni, Miswaki , dawa za meno, pamoja na nguo zengine za wazazi ambao ni wauguzi wa watoto hao vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh.1.5Millini.


Aidha Pia wametoa pesa taslimu Tsh.1,200,000 kwaajili ya kugharamia matibabu ya mtoto mmoja ambaye ni mdogo kuliko wotw kwenye wadi hiyo.


Doreen ametoa wito kwa watanzania kuwa na moyo wa kuwasaidia watu wanao ishi kwenye mazingira magumu wajane na wagonjwa ili na wao waweze kufarijika. Misaada muhimu inayohitajika kwa wau hao ni Chakula zaidi na gharama za matibabu.

Wadi hiyo in jumla ya watoto 60 ambao wamelazwa wakiwa na wazazi wao.Mwenyekiti wa kikundi hicho Doreen akimbeba mtoto ambaye amelazwa kwenye wadi ya tumaini mara baada ya kutoa msaada.

No comments: