Sunday, May 20, 2012

YANGA WASHAMBULIA WABUNGE NA VINGOZI WA SERIKALI.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usuluhishi ya Vijana wa Yanga akiwahutubia vijana wa Yanga waliokusanyika kwenye Kiwanja Cha Klabu hiyo Jangwani jijini Dar es Salaam leo, na kutangaza mikakati mbalimbali ya kuimarisha klabu yao.DAR ES SALAAM
UMOJA wa vijana wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, umefanya mkutano wa aina yake kwenye Uwanja wa Kaunda uliopo klabuni hapo na kuwashambulia wabunge na vingozi wa Serikali ambao ni mashabiki wa Klabu hiyo.

Vijana hao wamesema wamechoshwa na vingozi hao ambao ni mashabiki wa klabu hiyo lakini hawajitokezi hadharani kama wanavyojitokeza na kujipambanua waziwazi viongozi ambao ni mashabiki wa wapinzani wao Simba.

mkutano wa wanachama vijana utakaofanyika leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo kuanzia saa 8:00 mchana kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kipigo cha magoli 5-0 walichokipata Jumapili iliyopita kutoka kwa watani zao Simba.

Akifafanua Mwenyekiti wa Umoja huo Bakili Makele anasema viongozi wa Serikali na Wabunge karibu wote ukiondoa wachache wanaoweza kujipambanua wazi wazi mbele ya jamii kama wao ni mashabiki wa yanga tofauti na wanavyofanya viongozi wanaoshabikia Simba.

Akiwataja baadhi ya Wabunge, Makele alisema kuna Mze Kapuya, Zito Kabwe, Murtaza Mangungu na Hata hayati Mzee Kawawa alikua akijipambanua waziwazi lakini wako wapi wanaoshabikia yanga? alihoji Makele.

Mbali na tukio hilo viongozi hao wanaendelea na mchakato was kutaka kumg'oa uongozini Mwenyekiti wa Klabu hiyo Royd Mchunga, baada ya kufanya uamuzi wa kukusanya saini za wanachama wanaompinga na kuziwasilisha TFF, kwa kutokuwa na imani na kiongozi huyo, 'Hadi raha za Pwani' inatoka eneo la tukio Jumla ya Saini za wanachama 693 zimekwisha sainiwa.

Idadi hiyo ya Saini imezidi ile idadi iliyokuwa ikihitajika ya watu 500 wakumpinga mwenyekiti huyo.

Katika hatua nyingine klabu hiyo imetangaza kuanza kwa zoezi la usajili wa msimu mpya wa ligi hapo kesho huku ikibainisha kuwa wachzaji 13 mikataba yao imemalizika akiwemo Nadir Haroub Kanavaro.
 
 Mwanachama Mkongwe wa Klabu ya Yanga na Mzee wa timu hiyoYusuph Mzimba, akiwahutubia wanayanga hao waliokutana kujadili mambo mbalimbali ya Klabu yao.
 Baadhi ya Wanachama wa Klabu hiyo.
 Wanachama wakiwapigia makofi viongozi wao.
                                              Mwenyekiti wa Wazee wa Yanga Mze Akilimali.
 Mashabiki waoo walikua Nyuma ya Ukuta wa Uwanja huo wa Kaunda maeneo ya Jangwani wakifuatilia Mkutano huo, kwakua wao si wanachama hawakupaswa kuhudhuria, ila walifuatilia kwa makini

Mandhari ya eneo la mkutano ilivyokuwa.

No comments: