Saturday, January 26, 2013

CHANZO CHA VURUGU ZA LEO MASASI HIKI HAPA!

CHANZO cha vurugu za leo Mkoani Mtwara imeelezwa kuwa ni askari wanaozinguka mjini na pikipiki maarufu kwa jina la Tigo baada ya kumkamata dereva wa pikipiki na kuanza kumpiga.  

Madereva  wenzake walipoona tukio hilo la mwenzao kupigwa waliingilia kati mzozo huo na kumtoa mwenzao kwenye kadhia hiyo. 

Baada ya kumtoa mwenzao kundi la madereva hao wa bodaboda waliandamana hadi kituo cha Polisi wilayani humo ili kueleza hisia zao lakini walipofika polisi walianza kuwafyatulia mabomu yakutoa machozi yalioibua hasira za wananchi na kuanza kusogelea eneo la kituo hicho badala ya kukimbia. 

Wananchi hao walijazana kwenye kituo hicho huku polisi wakiendelea kupiga mabomu lakini polisi walionekana kushindwa na wananchi wakapata nguvu na kuanza kuchoma moto magari ya halmashauri na majengo.

  Baada ya kutoka hapo walielekea kwenye nyumba ya Mbunge wa jimbo hilo wakaichoma moto wakaenda kwenye ofisi ya serikali ya mtaa, kwenye tawi la chama cha mapinduzi na baadaye kwenda kwenye nyumba ya Mwenyekiti wa bodi ya Korosho Mama Anna Abdalla.    

Kwamujibu wa mmoja wa wananchi wa Masasi aliyejitambulisha kwa jina la Mussa amesema ameona magari manne yakiwa na majeruhi wa tukio hilo wakikimbizwa kwenye Hospitali ya Ndanda.

Aidha Mganga mmoja wa Hospitali ya Wilaya akizungumza na kituo kimoja Cha Radio alisema kuwa hospitalini hapo wamepokea miili ya watu watatu lakini amesema kuna uwezekano mkubwa idadi ya watu waliokufa ikawa kubwa zaidi kwasababu wapo wengine wamechukuliwa na nduguzao hukohuko kwenye matukio.

1 comment:

Anonymous said...

Hivi kweli kuna uhusiano wowote wa tukio hili la kuchoma nyumba na magari na kitendo kilichotokea kati ya derva wa bodaboda na polisi?! Nadhani there is a hiden agenda in this issue! Wananchi wa kusini hebu tutafakari kwa makini,je hizi ofisi za serikali tunazoziharibu leo hatutazihitzji kesho ka huduma zetu?! Hatutahitajio huduma za upimaji wa viwanja? Hatutahitaji huduma za elimu au mahakama? Tutafakari kabla ya kutenda huku tukielewa kuwa TWO WRONGS DOESNT MAKE IT RIGHT!