Sunday, January 27, 2013

KAMATAKAMATA YAENDELEA MASASI MABOMU YAANZA KUSIKIKA MCHANA HUU!

BAADA ya watu Saba akiwemo askari polisi mmoja kuawa katika vurugu zinazoendelea wilayani Masasi mkoani Mtwara, zikiwazimebeba sura ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam kinachoendelea saivi ni kamatakamata ya watu aliyekuwemo na asiyekuwemo.

Taarifa za kufariki watu saba zimethibitishwa na Muuguzi wa zamu hospitali ya wilaya ya Masasi, Mkomaindo Fatuma Timbu ambaye alisema wamepokea maiti hizo za watu saba.

Aidha majeruhi ambao idadi yao haijajulikana wamekimbizwa hospitali ya misheni ya Ndanda kwa matibabu na hali bado ni tete kutokana na vurugu kubwa zilianza majira ya saa 4 asubuhi  jana. Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea juu ya hali inavyoendelea.

No comments: