Saturday, January 26, 2013

LAANA YA GESI IMEWAHI KUTOKEA, Tumshukuru mungu kwa kuwahi kutokea!


NILIWAHI kusikia kwa kiongozi mmoja wa dini alisema hivi “Mnaweza  mkalipenda jambo na mkaling’ang’ania hali yakua jambo hilo linamadhara kwenu lakini hamjui na mnaweza mkalichukia jambo kwa nguvu kubwa kumbe ndio lenye faida kwenu” mwisho wa kunukuu.

Hakuna mtu anaependa kuona vurugu zikitokea mahala popote kwani mali na maisha ya watu hupotea kama sio kupoteza viungo vya mwili na kupata ulemavu wa kudumu. Lakini kwa mgogoro huu tumshukuru sana mwenyezmungu kwa kutokea wakati huu kuliko ungetokea wakati miundombinu ya mradi wa gesi ikiwa imekwisha jengwa (Laana ya gesi imetuwahi mapema kabla).

 Pamoja nakwamba wataalamu wanaeleza kua gesi asilia haina athari sana ya milipuko ikilinganishwa na aina nyingine za gesi lakini siku kama yaleo tungekuwa tunazungumza janga la Afrika ama la Kidunia maana na hakika kwa hasira walizokuwanazo vijana wa Mtwara wasingeshindwa kwenda kulipua moto bomba la gesi.

Kama hilo lingefanyika bilashaka tungelishuhudia moto ukitoka Mtwara kuelekea jijini Dar es Salaam kuliangamiza jiji lenye wakazi zaidi ya 5Millioni. Hapa watanzania tumepata funzo kwenye tukio hili na tujifunze kutokana na makosa.

KWANINI MATUKIO YA FUJO YAMETOKEA SASA MTWARA? Majibu ya swali hili niwazi sababu kubwa ya matukio hayo ya vurugu ni serikali yenyewe kwakushindwa kushughulikia tatizo la msingi badalayake iliendelea na tabia ya kuwa na majibu rahisi kwenye maswali magumu yanayoaambatana na kejeli.

Majibu ya kejeli ya serikali kupitia mawaziri wake na hata viongozii wa chama tawala wa mkoa huo wamechangia kupandisha hasira kubwa zilizokosa mtu wakuzishusha kwakutoa majibu ya kuleta matumaini kwao kabla ya kuanza kutoa elimu kwa wananchi hao. Kwakua hakuna aliyekwenda kuwapa elimu yoyote kuhusu yale madaiyao ilitosha ujumbe wa upande mmoja wanaoupata kujaza ‘vakyum’ na kusubiri ipasuke tu.

Pamoja na hasira za wananchi hao kuwa nyingi na kuonekana waziwazi kwamba wanatafutia sababu tu ili waonyeshe hasira zao bado serikali ilikua kwenye usingizi mzito nakujisahau kabisaaa, hata pale wanasiasa walipokwenda kunyunyizia petrol mgogoro huo hakuna aliyejali kwenda kuondoa tatizo.

Alianza Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia akaonja vurugu walipomkatalia hojazake akajinasibu kisiasa kuwa ni kikundi cha watu wachache tu ndio wanaleta fujo lakini wengiwao wamemuelewa.

Wakaja watu watanesco walipozima umeme wakati mkutano wa wanasiasa wa upinzani ukiendelea, na mabomu yakapigwa bado serikali ikapuuzia tu.

Akachomewa moto gari Afisa wa usalama wa Taifa, bado tukaona kimya.

Akavamiwa diwani kwa madai ya ushirikina na tukio la mwisho lililosababisha vifo vingi vya watu sita jana Chanzo ni Polisi kumshikilia mwendesha bodaboda. Utaona ni wazi hawa wananchi walikua na presha ambayo ikitafuta sehemu ya kutokea tu na hili lilishabainika na wachambuzi wa mambo ya kijamii. Nathubutu kusema laana ya gesi imewahi kabla ya muda ili tujifunze kwanza na namna ya kukabili matatizo yatakayokuja kujitokeza baadaye maana ni lazima yatokee kwasababu waswahili walishasema kwenye riziki hapakosi fitina. UCHAMBUZI WA MHARIRI RAHA ZA PWANI.

No comments: