Wednesday, January 30, 2013

MAPINDUZI CUP WAKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Mapinduzi CUP ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar, kupata nasaha pamoja na kukabidhi vyeti vya Shukurani kwa wahisani waliochangia kufanikisha mashindano ya Kombe la Mapinduzi CUP.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Mapinduzi CUP na Wahisani waliochangia Kombe hilo, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa  akizungumza nao jana Ikulu Mjini Zanzibar, pia Kukabidhi Vyeti vya Shukurani kwa michango mbali mbali iliyotolewakufanikisha Mashindano hayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti cha Shukurani Mwakilishi wa Jimbo la Bububu na Meneja wa Ocean View Hotel, Hussen Ibrahim Makungu, kwa Mchango wa Hoteli yake  kuchangia Kombe la Mapinduzi Cup,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.

No comments: