Sunday, January 27, 2013

MEYA WA KINONDONI AHAMASISHA USAFI JIJINI DAR LEO.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amefanya ziara ya uhamasishaji utunzaji wa usafi wa mazingira kwa wakazi wa kata ya Ndugumbi, jijini leo (Jan 27). Pamoja na Mambo mengine ameahidi kuwa zoezi hilo litakuwa ni endelevu ambapo kila mwisho wa wiki, wakazi wanaoishi kwenye Kata mbalimbali za Manispaa hiyo watakuwa wakitekeleza zoezi hilo. Pichani ni zoezi hilo lilivyotekelezwa leo kwa viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (Suruali ya njano) akisimamia uondoaji wa taka zilizokuwa zimetelekezwa pembezoni mwa Barabara ya Mandela.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda sambamba na viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi wakisafisha na kuzibua mitaro katika Mtaa wa Ndugumbi.

No comments: